TANZANIA YAJINASIBU KUJIKITA KILIMO CHA BIASHARA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 10 July 2021

TANZANIA YAJINASIBU KUJIKITA KILIMO CHA BIASHARA.

 


Serikali imejikita katika kuimarisha utafiti juu ya kilimo kwa lengo la kuhakikisha inafanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuondokana na dhana ya kilimo cha kujikimu na kuhamia cha biashara.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Kilimo,Profesa Adolf Mkenda,Tarehe 9 Julai 2021,alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Profesa Mkenda,alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa Serikali ya Tanzania kupitia  Wizara ya Kilimo imejipanga kufanya mageuzi hayo kwa kujikita zaidi katika utafiti utakaokuwa msaada katika kuongeza tija katika Kilimo.

Alisema kuwa maendeleo ya kilimo yanategemea zaidi utafiti hususani wa udongo vilevile kubaini teknolojia bora itakayo pelekea kukisogeza kilimo katika hatua kubwa ya mafanikio na kimageuzi.

Aliendelea kusema kuwa pamoja na mambo mengine wizara ya kilimo pia imejipanga katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kuliko kusafirisha pasina kuongeza thamani,hatua itakayosaidia uchumi wan chi kuapanda na kuongeza soko la ajira nchini.

“…. tutakuwa na Pato zuri la kigeni sambamba na utambulisho wa nchi” Alikaririwa Profesa Mkenda.

Aidha alitoa wito kwa wadau kujitokeza kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji,kutokana na sekta ya kilimo kujipanga katika kilimo hicho cha umwagiliaji nchini,kwa kutanabaisha kuna Hekta zaidi ya Milioni 29,zilizotengwa kwa kilimo hicho huku hekta Milioni moja tu ndizo zinazotumika kwa kilimo hicho cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Andy Karas,aliipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso