Mkazi wa mtaa wa Matema,kata ya Maguvani,mjini Makambako,Eliza Mangita,amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa katika kibanda chake cha biashara.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issa,alisema tukio hilo lilitokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwawahi wateja wake wa asubuhi.
Aidha kamanda Issa aliwataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili kuiokoa jamii.
Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.
No comments:
Post a Comment