Watu sita wameripotiwa kufariki katika vurugu zinazodaiwa kusababishwa na kufungwa kwa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
Wanajeshi wamelazimika kuingia mitaani ili kudhibiti vurugu zinazoendela ambapo hadi sasa watu 219 wamekamatwa katika vurugu hizo.
Katika Jimbo ambalo Zuma anatokea, KwaZulu Natal kumekuwa na fujo nyingi ikiwemo raia kuchoma maduka, vurugu ambazo zilianza mara baada ya Zuma kujisalimisha polisi ili kutumikia kifungo cha miezi 15.
Hukumu dhidi ya Zuma ambayo ni ya kwanza dhidi ya rais wa zamani wa nchi huko Afrika Kusini, ilizua mtafaruku wa kisheria na kufuatiwa na maandamano makubwa ya wafuasi na watetezi wa mwanasiasa huyo.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alilazimika kujiuzulu mwezi Februari mwaka 2018 kutokana na mashinikizo ya chama tawala cha ANC kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka yake.
No comments:
Post a Comment