IMEFAHAMIKA kwamba uongozi wa Kata ya Segese,katika Halmasahuri ya Msalala,wilaya ya Kahama,imefikia hatua ya kuomba huduma za Kibenki, kutokana na Kata hiyo kushamiri kwa shughuli za kibiashara zinazochagizwa na wingi wa wachimbaji wadogo wadogo madini ya dhahabu katika maeneo hayo.
Kata ya Segese ipo umbali wa kilometa 40
kutoka Kahama Mjini,kwenye huduma za kibenki,huku Kata hiyo ikiwa na mzunguko
mkubwa wa kifedha,hivyo kuomba ngazi husika kuangalia uwezekano wa kufungua
tawi dogo la Benki kurahisisha huduma za fedha mahali hapo.
Hayo yalibainishwa juzi na Mtendaji wa Kata ya Segese, John Mahona, wakati akiongea na Waandishi habari,juu ya usalama wa fedha ambazo wanakuwa nazo wachimbaji hao katika eneo hilo huku wengine wakitumia mabegi na mifuko badala ya kuweka katika taasisi za kifedha.
Mahona alidai eneo hilo lina mahitaji makubwa ya huduma za kifedha kwa ajili ya usalama wa Wachimbaji madini ya dhahabu, wanaopata tabu kupata huduma za kifedha za kibenki na kulazamika kutembea umbali huo jambo ambalo linahatarisha maisha yao.
Mahona alisema kuwa katika kaya yake mbali na
wachimbaji hao kumiliki fedha nyingi pasipo ulinzi wake pia kuna maduka mengi
ya fedha fedha ambayo kimsingi wamiliki wake wamekuwa wakiaa na fedha nyingi
bila ya kuhofoa usalama wao.
“….tuna mzunguko mkubwa wa fedha kutokana na
madini yaliyopo,ni muhimu kukawa na tawi lolote la kibenki kwa usalama wa watu
wa eneo hili,”alisema Mahona.
Hata hivyo Mtendaji huyo, alisema kumekuwa na
ongezeko kubwa la watu kutoka 20,000 hadi kufikia
35,000 kutokana na machimbo hayo ya Ntambalale namba moja hadi tano
ambayo watu wengi wanachimba madini ya dhahabu katika maeneo hayo.
Aidha alisema kuwa machimbo hayo yamesaidia
pia kukuza uchumi kwa watu na mtu mmoja mmoja katika eneo hilo huku akiongeza kuwa
hali hiyoimetokana na baadhi ya wachimbaji wadogo kupewa Leseni za uchimbaji
katika maeneo hayo.
Alisema kuwa wachimbaji hao wameweza kusaidia
katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika Kata ya Segese kama vile
kujenga kwa gharama zao Zahanati katika kijiji cha Wisolele na kuongeza
kuwa pia wamejenga kituo cha Polsi katika Mji wa Segese.
Aliendelea kusema kuwa pia wachimbaji hao wameshiriki katika ujenzi wa vyoo vya matundu sita katika Shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere,kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Segese na kusaidia ukamilikaji wake wa jengo la utawala.
No comments:
Post a Comment