SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEZINDUA RIPOTI YA PILI YA UCHAMBUZI WA BAJETI ZA LISHE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 18 June 2021

SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEZINDUA RIPOTI YA PILI YA UCHAMBUZI WA BAJETI ZA LISHE

 Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndungai Leo amezindua ripoti ya pili ya Uchambuzi wa bajeti za lishe kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika 2020. Uchambuzi huu wa Bajeti za lishe umefanyika katika nchi 8 ambazo ni Tanzania, Malawi, Kenya, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Ethiopia na Rwanda)


Lengo kuu la Uchambuzi huu ni kuzisaidia nchi wanachama kuunda na kutekeleza bajeti ambazo zinalenga kufikia malengo ya ajenda za lishe ulimwenguni, kikanda na nchi husika. Ripoti hii pia inalenga katika kutambua changamoto katika upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya afua za lishe hususani kutoka vyanzo vya ndani katika nchi husika kwa lengo la jujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

Uzinduzi huo ulihudhuliwa na Waheshimiwa Wabunge wanachama wa kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe na Usalama wa Chakula na Haki za Watoto Bungeni. Sambamba na uzinduzi huo, Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kusikiliza na kujadili hali ya lishe nchini, na jitihada zilizofanywa na sekta mtambuka katika kuboresha hali ya lishe nchini.

Kikao kiliandaliwa na PANITA na ASPIRES kwa kushirikiana na Graça Machel Trust (GMT) na Care International kupitia Shirikisho la mitandao ya Asasi za kiraia zinazofanya kazi za Lishe Mashariki na kusini mwa Afrika (East and Southern Africa Nutrition Civil Society Alliance.

SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JOB NDUNGAI WAKATI WA UZINDUZI WA RIPOTI YA LISHE.

KAMATI YA BUNGE IKIONGOZWA NA MH SPIKA PAMOJA NA MKURUGENZI WA PANITA KATIKA UZINDUZI WA RIPOTI YA LISHE


MKURUGENZI MTENDAJI WA PANITA NDUGU TUMAINI MIKINDO AKITOA NENO NA UFAFANUZI KATIKA UZINDUZI WA RIPOTI YA LISHE.


SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JOB NDUNGAI AKIZINDUA RASMI RIPOTI YA LISHE.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso