MKUTANO WA UTALII AFRIKA WAFANYIKA TANZANIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 17 June 2021

MKUTANO WA UTALII AFRIKA WAFANYIKA TANZANIA






Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro ambao upo mjini hapa kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia masuala ya Utalii Duniani [UNWTO], ambao ni mahususi kwa nchi za Kiafrika kuweza kujadili na kufanya tafakuri kwa jinsi gani sekta ya Utalii itakavyorejea kwenye mstari wake baada ya kushambuliwa na madhara ya ugonjwa wa UVIKO 19, ambapo Tanzania mkutano ujao imekubaliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Waziri Ndumbaro amesema kuwa, ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida mbalimbali sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za utalii wa Tanzania katika mkutano huo ambao una Watalaamu Wabobezi Utalii Duniani

‘’Tumekutana nchi nyingi za Kiafrika, tumejadili mambo mengi, tumebadilishana uzoefu mkubwa tumepata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni ambayo yana uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii Duniani” Ndumbaro

Lakini pia tumepata fursa ya kufanya vikao vya ana kwa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala ya Utalii wa umoja wa Mataifa, Zurab Pololikashvili, tumezungumza naye vizuri kabisa na pia amekubali mkutano ujao wa utalii Barani Afrika ufanyikie Tanzania’’ Ndumbaro

Ndumbaro ameongeza kuwa, Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii baada ya UVIKO 19.

‘’Lakini muhimu zaidi, tumeweza kuomba na kukubaliwa kuiingiza Tanzania kuwa moja kati ya nchi tatu barani afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii. Nchi zingine zikiwa Namibia na Cape Vede ambazo zimeshaingizwa toka zamani kwa namna ya kipekee Tanzania tumepewa upendeleo huo baada ya kushiriki hapa na tayari tutaingizwa katika mradi huo mkubwa…’’ Ndumbaro.

Aidha, amesema Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umepata utaalam na uzoefu mkubwa kwa jinsi gani watakavyoweza kunasuka na ugonjwa huo wa UVIKO 19, amewapongeza watanzania kushiriki na kuweza kufanikiwa.

Katika mkutano huo, leo 16 Juni kutakuwa na Mawaziri 15 kutoka nchi 15 za Afrika ikiwemo Tanzania wapata nafasi ya kuziongelea nchi zao katika mkutano ambao utarushwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali za ndani na nje ya Namibia ikiwemo mitandao ya Kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso