KATIBU TAWALA WA MANISPAA YA IRINGA AWAASA WAZAZI KUWAPA WATOTO CHAKULA KIZURI SIYO KUWAACHIA MAKOMBO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 18 June 2021

KATIBU TAWALA WA MANISPAA YA IRINGA AWAASA WAZAZI KUWAPA WATOTO CHAKULA KIZURI SIYO KUWAACHIA MAKOMBO

 Katibu Tawala wa Manispaa ya Iringa Ndugu Epstomy Kyando amewaasa wazazi kuwalinda watoto wao na kuwaendeleza kimasomo kwani Serikali inachangia gharama za masomo kwa kila mtoto toka Darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.


Ndugu kyando ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Mtoto wa Africa yaliyofanyika tarehe 17 Juni 2021 katika Shule ya Msingi nyumba tatu katika Manispaa ya Iringa.

Pia amewataka Wazazi kuacha tabia ya kula chakula chote na kuwapa makombo watoto wao ambapo wazazi hao wanakula chakula kizuri na kuwaachia mabaki ya chakula na kusababisha watoto kuwa na utapiamlo.

Watoto kutoka Shirika La Compassion wakitoa ujumbe wa siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Iringa.

Baraza la Watoto la Manispaa ya Iringa wakitoa ujumbe baada ya Igizo lao la kuhusu kupinga mimba za utotoni

Mjumbe kutoka dawati la jinsia akitoa ujumbe wa siku ya mtoto wa Afrika kwa kuelimisha juu ya haki za mtoto katika jamii.

Meza kuu katika Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika katika Manispaa ya Iringa

Katibu Tawala wa Manispaa ya Iringa Ndugu Epstomy Kyando akitoa hotuba katika maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika manispaa ya Iringa katika viwanja vya shule ya Nyumba tatu.


Umati wa wananchi na Watoto walioshiriki maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Africa manispaa ya Iringa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso