WATU SABA WAFARIKI BAADA YA KUTUMIA CHANJO YA ASTRAZENECA UINGEREZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 3 April 2021

WATU SABA WAFARIKI BAADA YA KUTUMIA CHANJO YA ASTRAZENECA UINGEREZA




Watu saba wamefariki nchini Uingereza kutokana na damu kuganda mwilini baada ya kupewa chanjo ya Oxford-AstraZeneca, mamlaka ya kudhibiti dawa imethibitishia BBC.

Kwa ujumla wato 30 kati ya milioni 18 waliopewa chanjo hiyo kufikia Machi 24 wamekabiliwa na hali ya damu kuganda.

Bado haijulikani ikiwa ni bahati mbaya tu au athari ya kweli ya chanjo.

Shirika la udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya linanasema faida ya chanjo zinaendelea kuzidi madhara yake.

Hata hivyo, hali ya kuganda kwa damu kwenye ubongo, kitaalamu "cerebral venous sinus thrombosis" au CVSTs zimesababisha nchi nyingine - zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Canada - kudhibiti utumizi wa chanjo hiyo.

Shirika la Afya duniani na Wakala wa Dawa wa Ulaya wanasema faida za chanjo hiyo huzidi hatari zozote.

Data zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa (MHRA) siku ya Ijumaa, zilionesha kuwa watu 22 walipata hali ambayo kwa lugha ya kimatibabu inafahamika kama cerebral venous sinus thrombosis (CVST) ambayo ni aina fulani ya mgando wa damu kwenye ubongo.

Hii ilifuatiwa na na viwango vya chini vya seli, zinazosaidia damu kuganda, mwilini. MHRA pia ilibaini watwengine wanane walikabiliwana tatizo la damu kuganda mwilini.

Sasa MHRA imethibitishia BBC kupita barua pepe, kwamba "inasikitika watu saba wamefariki "

Via BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso