Wanawake Mkoani Shinyanga wameshauriwa kuendelea kushirikiana na akinababa kufanaya kazi kwa bidii bila kukata tama ili kuleta maendeleo ya familia katika mkoa huo.
Hayo yalisemwa na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Zainabu Telaki wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniania yaliyofanyikia katika viwanja vya ulowa Wilayani Ushetu iliyopo Mkoani humo
Alisema akina mama wasiwe tegemezi kwa akina baba washirikiane kwa pamoja kufanya kazi ili watengeneze familia bora kwa maendeleo yao ya baadae
‘Walezi wote wanawajibu wa kusimia malezi ya watoto wao na kuangalia maadili ili kupunguza mambo ya ukatili ubakaji uzalilishaji katika mkoa huo. Alisema Telaki.
Nao baadhi ya akina mama waliokuepo kwenye maadhimisho hayo wali sema watahakikisha wanasimamia familia na malezi bora katika familia zao na kufanya kazi kwa bidii ili kuepusha migogoro ya marara kwa mara katika familia kwa kushirikiana na akinababa.
‘Walezi wote tunawajibu wakufanya kazi kwa bidii na kuendesha familia zetu katika msitari ambao una maadili uli kuwakomboa watoto wetu kwani ndio taifa letu la kesho.Alisema Amina Iddy.
Naye Martine Makoye akizungumza kwa niaba ya akinababa alisema kuwa ata shirikiana na familia yake kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo bora kwenye familia na hata taifa.
No comments:
Post a Comment