WAGONJWA ZAIDI YA 1000 WANAHITAJI FIGO NCHINI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 15 March 2021

WAGONJWA ZAIDI YA 1000 WANAHITAJI FIGO NCHINI.


ZAIDI wa wagonjwa 1000 nchini wanahitaji huduma ya upandikizaji figo, lakini changamoto kubwa ni kupata watu ambao vipimo vitaendana na mgonjwa husika.

Hayo yamesemwa na Rais wa Chama cha Wataalamu wa Figo Tanzania, ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Onesmo Kisanga na kudai kuwa kwa sasa kunauhitaji mkubwa wa upandikizaji figo nchini.

Dk Kisanga amebainisha kuwa ugonjwa wa figo uko kwa asilimia 10 kwa ukanda wa jangwa la Sahara huku utafiti wa ngazi ya jamii uliofanywa kaskazini mwa nchi kwa Mkoa wa Kilimanjaro ukionesha asilimia 6.7 ya watu wanatatizo la figo sababu ikiwa ni ukosefu wa elimu.

“Changamoto ni kupata watu wanatoa figo hapa panakuwa pagumu kwasababu  ni lazima figo inayotolewa  iwe salama na mnakubaliana na kuna vipimo ambayo vinayoendana na mgonjwa wakati mwingine ndugu  anaweza kupatikana lakini vipimo vikifanyia haendani na mgonjwa." alisema Dk Kisanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso