Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Generali John Mbungo amejinasibu kwa mwaka 2019/2020 kufanikiwa kutekeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa 89.8% tofauti na asilimia 88.1 walizofikia mwaka 2018/2019.
Mbungo alibainisha hayo wakati akikabidhi ripoti yake kwa Rais, Samia Suluhu
Hassan,Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma,ambapo alibainisha mafanikio hayo
yamekuja kutokana na elimu kwa umma wanayotoa TAKUKURU.
Alisema mafanikio hayo yamekuja kutokana na kutoa elimu kwa umma kuhusiana na
madhara ya rushwa kwa wananchi ambapo semina zipatazo 3683 zilitolewa na
kusaidia majalada 1079 kukamilika tofauti na mwaka uliopita ambapo yalikuwa
911.
“Kati
ya majalada hayo majalada 385 yalihusu hongo na majalada mengine 694 yalihusu
vifungu vingine vya sheria vya kuzuia na kupambana na rushwa” amesema Mbungo.
Aidha, amebainisha kuwa hadi majalada hayo uchunguzi wake
unakamilika uligusa sehemu mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa sheria ya manunuzi
ya umma, vyama vya ushirika vya masoko ya mazao ya kilimo kutowalipa wakulima
baada ya kuuza mazao yao kwenye vyama hivyo, mikopo umiza na ufujaji wa fedha
katika miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment