IMEELEZWA kwamba mila na desturi za jadi,zinazoabudiwa na baadhi ya wachimbaji wadogo,zimekuwa ni miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kuibuka kwa magonjwa ya milipuko kipindi cha masika katika maeneo ya migodi.
Hayo yalielezwa na Katibu wa Idara ya Afya na
Mazingira,katika Mgodi wa madini ya dhahabu wa Mwime Two,Veronica Paul,kwa
kubainisha kwamba kuna baadhi ya wachimbaji madini ambao hawana desturi ya kujisaidia
haja kubwa na ndogo katika vyoo.
Veronica alisema baadhi ya watu wanaofika
kufanya shughuli za uchimbaji huamini mafanikio ya katika shughuli hiyo
hupatikana kwa kuamini kufanya vutendo vya jadi ambavyo huelekezwa kutofanya
vitendo Fulani ikiwemo kujisaidia ndani
ya vyoo,kusudi wapate mafanikio.
Alisema utamaduni huo huwafanya kuwa na
desturi ya kujisaidia vichakani pasipo kujali kuwa tabia hiyo inaathiri afya
zao hasa kipindi cha masika ambapo kinyesi wanachokitoa na kutokihifadhi eneo
husika kinaweza kuwasababishia maradhi ya milipuko.
“..tumewahi kuwakamata watu kadhaa
wakijisaidia vichakani,wakadai ndio maelekezo waliyopatiwa wakati wakiagwa na
bibi kuja kutafuta mali,kuwa ni marufuku kujisaidia ndani ya choo,”alisema bi
Veronika.
Hata hivyo alisema wamekuwa na dhamira kubwa
ya kutoa elimu ya usafi na mazingira kwa wachimbaji hao lakini kikwazo
wanachokutana nacho ni wachimbaji hao kutokuwa tayari kuhudhuria mafunzo kwa
madai yanawacheleweshea muda wa kutafuta mali.
Kwa upande wake Michael Kazimiri,mchimbaji mdogo katika machimbo ya Mwime,alisema kila mchimbaji anayefika katika mgodi huo huamini imani za jadi kuwa ndizo zitamletea mafanikio,hivyo ni budi watekeleze masharti wanayopewa na wataalamu wa mila kabla hawajafika migodini.
No comments:
Post a Comment