WANAWAKE nchini wenye ajira Serikalini na kwenye Taasisi mbalimbali za umma wameaswa kuwa na maono chanya katika kutekeleza majukumu yao ili kuliletea tija taifa sambamba na ufanisi wenye mabadiliko makubwa katika maisha yao ya kila siku.
Pia wanatakiwa kuzingatia weledi mkubwa,uadirifu na uwajibikaji uliotukuka wenye maono katika jamii inayowazunguka katika utekelezaji majukumu yao ngazi ya familia,pindi wanapowajibika katika idara mbalimbali binafsi,za taasisi za umma ama serikalini.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Meneja Mkaguzi kutoka Mamlaka
ya Mapato (TRA) Mkoa wa kikodi wa Kahama,Irene Hance, wakati akiongea na Waandishi
wa habari ofisini kwake ikiwa ni kilele cha siku ya wanawake Duniani,ambayo mkoa
wa Shinyanga uliyaadhimisha wilayani Kahama.
Hance alisema pamoja na uwepo wa mabadiriko
ya kidunia,bado hayatamuondoa mwanamke kujitambua kuwa anawajibu katika malezi
ya familia,na kushauri kuwa na uwajibikaji wenye tija kwa taifa pasipo kuathiri
majukumu yao ya nyumbani kama mama,kwa ustawi wa kizazi kijacho.
“ Pamoja na utumishi wetu
serikalini,tunapaswa majukumu ya nyumbani tuyatekeleze,tujiheshimu na kumpa
haki yake mwanaume ambaye ndiye kichwa cha familia ili tumudu kutoa malezi
yenye maadili katika familia zetu,”alisema Hance.
Aidha alionya jamii ya Kanda ya Ziwa
kuendeleza Mila na Desturi potofu juu ya mtoto wa kike,kumgeuza mtaji wa
familia kwa kumuozesha katika umri mdogo na kumnyima haki yake ya msingi kupata
elimu ambayo ndiyo msingi wa maisha yao.
Alikumbusha umuhimu wa mtoto wa kike
kuendelezwa kielimu kwakuwa ni msaada mkubwa katika jamii,hivyo kuwaingiza
katika ndoa mapema ni kuwanyima haki zao za msingi kuja kuwajibika kikamilifu
katika majukumuya yenye tija na taifa na familia zao.
Hata hivyo alibainisha kuwa pamoja na
mwanamke kutakiwa kujitegemea kwa kina katika uwajibikaji wake na kufikia
mafanikio hadi ngazi ya kusaidia familia,ambapo mafanikio yake hayapaswi
kutenganishwa na mwanaume kwakuwa hutegemeana katika kutekeleza majukumu.
Meneja huyo Mkaguzi kutoka TRA alitoa wito kuwaheshimu waume zao pindi wanapopata madaraka na kuongeza kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu amewawakilisha vizuri katika kutumikia uongozi wa umma katika kipindi chote cha uongozi wake
Kwa upande wake Mjasiriamali kutoka Kata ya
Mhungula,Halmashuri ya Manispaa ya Kahama, Zilpa Madaha,alisema baadhi ya wanaume
wamekuwa wakiwazuia wake zao kufanya kazi au Biashara kwa kile walichodai kuwa
wanaweza kuwazidi kipato hivyo kazi yao kubwa ni kulea watoto nyumbani.
Madaha alisema kuwa wanaume wamekuwa na wasiwasi Mkubwa wakisikia Mwanamke anataka kujiendelezaa kufanya biashara hali ambayo kwa maisha ya sasa muhimu katika familia ni kusaidiana katika kutekeleza majukumu yanayohusu familia kwa kila mmoja kuwajibika kwanafasi yake.
No comments:
Post a Comment