Hayo yalibainishwa juzi wilayani Kahama,na timu ya Wataalamu wa Serikali na Muwekezaji wa Kampuni ya Tembo Nickel itakayochimba madini hayo,waliofika kuangalia na kubainisha eneo sahihi linalostahiki kujengwa Mtambo huo wa kuchenjua madini hayo yanayochimbwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Akiongea baada ya kubaini eneo sahihi,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kabanga Nickel,Chris Showalter,alisema kukamiilka kwa ujenzi wa Kinu hicho,watu zaidi ya 1000,wanatarajiwa kuajiriwa katika Smalter hiyo itakayojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi katika halmashauri ya manispaa ya Kahama.
Aidha Showalter alisema uwekezaji huo kampuni ya Tembo Nickel,utanufaisha ajira takribani 2000 katika wilaya ya Ngara,mkoani Kagera mara shughuli za uchimbaji wa madini ya Nickel utakapoanza.
Kabla ya kuelekea kuangalia maeneo yaliyotengwa kwa ujenzi wa Smalter hiyo,Kamishina wa Tume ya Madini Nchini,Profesa Abdulkarimu Mruma,aliyekuwa ameongoza timu ya Wataalamu wa madini,alisema eneo hilo limetengwa katika uwekezaji wa Mgodi wa Buzwagi ili kurahisisha usafishwaji wake baada ya kuchenjuliwa.
Profesa Mruma alifafanua kwamba ilipendekezwa kujengwa kinu hicho wilayani Kahama kutokana na uwepo wa uwekezaji wa Migodi mikubwa ya madini ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu,na utatumika kuchenjua pia makinikia ya dhahabu badala ya kusafirishwa nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment