GGML YAZINDUA MFUMO RAHISI WA ULINZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 15 March 2021

GGML YAZINDUA MFUMO RAHISI WA ULINZI


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhili Juma (katikati) akionesha kipeperushi chenye maelezo ya namna ya kutoa taarifa za ulinzi na usalama kwa kampuni ya GGML

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML),imeimarisha mahusiano yake na jamii inayozunguka uwekezaji wao,kwa kuzindua na kutoa fursa kwa raia mwema kudhibiti uharifu kwa kupiga simu ya bure kwenye mfumo wa kutoa taarifa mbalimbali za ulinzi ,usalama na za kijamii.


Mfumo huo wa kidigitali, utawezesha raia wema wanaozunguka eneo la mgodi kupiga simu namba 0800 750 145 bila malipo yoyote,pindi  wanapobaini vitendo vya uhalifu vikiwemo kula njama, uharibifu wa mali za kampuni, vitendo vya rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi au wakandarasi wanaofanya kazi na kampuni ya GGML.


Akizindua mfumo huo mkoani Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhili Juma alisema teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu katika kipindi hiki ili kujibu changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwemo uhalifu na hujuma ya miundombinu mbalimbali ikiwemo umeme au mabomba ya maji ambayo huigharimu serikali fedha nyingi.


Aliipongeza Kampuni ya GGML,kwa ubunifu huo ambao utakaosaidia  serikali kupata taarifa mbalimbali za kihalifu kama vitendo vya kiusalama ikiwemo uendeshaji wa magari usio salama,na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa kuweka mazingira bora yatakayomlinda na kumuwezesha Mwekezaji  kufanya shughuli zake kwa ufanisi na usalama hivyo kutoa ajira na kuchangia pato la taifa  kupitia kodi na tozo mbalimbali. 


Akizungumzia mfumo huo, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya ulinzi kutoka Kampuni ya GGML, Suleiman Machira alisema mfumo huo umekuja kipindi muafaka wakati kampuni ya GGML na wakazi wanaouzunguka mgodi huo wakiwa wameimarisha mahusiano mema ya kindugu na kufanya shughuli zao kwa ushirikiano mkubwa. 


Machira aliongeza kuwa mwekezaji anapofanya shughuli zake kwa usalama bila kuhujumiwa au kufanyiwa vitendo vya kihalifu maana yake ataweza kufanya shughuli zake za uwekezaji kwa amani na kuchangia pato la uchumi wa mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla. 


Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, GGML imefadhili miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 30 katika kipindi cha miaka 3 katika mkoa wa Geita.


Hivi karibuni GGML pia imeibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini lakini ilichukua tuzo pia katika vipengele vya mazingira, usalama, mlipaji bora wa kodi, uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR) na uwezeshaji bora wa raia wa ndani ya nchi kwa mwaka 2019/2020.

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso