WANAFUNZIMSINGI NA SEKONDARI WASEMA ACHENI MILA POTOFU, TENDENI HAKI SAWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 10 February 2021

WANAFUNZIMSINGI NA SEKONDARI WASEMA ACHENI MILA POTOFU, TENDENI HAKI SAWA

 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameitaka jamii kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ili kusaidia kupinga ukatili wa kijinsia.


Wakizungumza katika warsha ya siku moja iliyowakutanisha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia Wazazi na wanafunzi, KATIKA ukumbi wa GAMA HOTELI ikiwa ni muendelezo wa juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto chini  ya ufadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOSIETY kwa kushirikiana na HUHESO FOUNDATION KUPITIA MRADI WA MWANAMKE AMKA ambao unaotekelezwa katika kata tano za manispaa ya kahama ambazo ni KINAGA, ZONGOMELA, MONDO, NGOGWA na KILAGO.

wanafunzi hao wamesema kuna baadhi ya tamaduni zinaendeleza ukatili kwa watoto wakike kunyimwa haki za msingi na wakiume kupatiwa kipaumbele.

 

Kwa upande wao maafisa maendeleo kutoka Kata ya Kilago na Mondo, Veronica Justine na Anna Tesha wamesema suala la wazazi kuhitaji mahari kubwa kipindi binti anapohitaji kuolewa imekuwa ni kichocheo cha kufanyiwa ukatili wa kijinsia wanawake.

 

Kwa upande wao wazazi wameahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kutoa taarifa za kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Aidha kuna jitihada mbalimbali za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kupitia mradi wa MWANAMKE AMKA ambao unafadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOSIETY kwa kushirikiana na HUHESO FOUNDATION na  unaotekelezwa katika kata tano zilizopo wilaya ya kahama ambazo ni KINAGA, ZONGOMELA, MONDO, NGOGWA na KILAGO.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso