Mume wa Spika wa bunge la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amehukumiwa kifungo cha siku tano jela baada ya kukiri kisa cha kuendesha gari huku akiwa mlevi.
Paul Pelosi, mwenye umri wa miaka 82, alikiri kuwa alikuwa amelewa pombe na kusababisha majeruhi baada ya kuligonga gari lake aina ya Porsche katika Kaunti ya Napa, California, katika mwezi Mei, 2022.
Kukiri kosa kwa Bw Pelosi, kulimuepusha milionea huyo kushitakiwa kwa kosa baya.
Pelosi ameoana na Bi Pelosi, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Democrat katika baraza la Congress la Marekani, tangu mwaka 1963.
Hatatumikia kifunguo zaidi cha jela chini ya makubaliano ya kukiri kosa.
Usiku aliokaa jela baada ya ajali tarehe 28 Mei utakuwa saw ana siku mbili. Siku nyingine mbili ziliondolewa kwa kuwa na mwenendo mwema, na siku ya mwisho atahudumu kwa kufanya kazi za manufaa ya kijamii kwa muda wa saa nane .
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment