Asilimia 39 ya Watanzania hawataki kulipa kodi wakihisi ni kubwa.
Hayo yamebainishwa katika ripoti ya Uchumi na Tozo iliyozinduliwa na Taasisi ya Twaweza leo Alhamisi Agosti 25, 2022.
Akieleza matokeo ya ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema asilimia 20 ya Watanzania wanaona wanalipwa mishahara modogo huku asilimia 15 wakihisi kodi hazitumiki vizuri.
"Asilimia tisa ni utamaduni wa jumla wa kukwepa kodi, asilimia sita wanaona adhabu sio kali na asilimia tano wanaona kuna uwezekano mdogo wa kukatwa na asilimia nane hawajui," amesema.
Aidha, ripoti hiyo inaeleza wananchi wengi wanasema hawajui asilimia 42 ya mapato ya tozo yanatumikaje kuliko wanaosema wanajua ambao ni asilimia 38.
Miradi inayotajwa zaidi ni elimu kwa asilimia 26, huduma za afya asilimia 25 na miundombinu ya barabara kwa asilimia 21.
Kwa upande mwingine, ripoti hiyo imeonyesha asilimia 56 ya Watanzania wanasema gharama za maisha zimepanda walipoulizwa Novemba 2021, huku Julai 22 asilimia 48 walisema hivyo.
No comments:
Post a Comment