Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari (kushoto) akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari (kushoto) akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
PICHA ZOTE NA MALUNDE
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa Internet (Intaneti) nchini huku ikiziomba serikali za Afrika ziweke mazingira wezeshi kwa wazalishaji wa maudhui wa ndani ya nchi kunufaika na wanachozalisha kutoka kwa wanaotumia maudhui yao ambao ni Google, Meta,Netflix, Sporty na wengine ambao ni wakubwa kwenye eneo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania MISA – TAN, Bi. Salome Kitomari wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Kitomari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA KANDA, na mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe linalomikiwa na Kampuni ya The Guardian Limited amesema MISA-TANZANIA inampongeza Rais Samia Suluhu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kututumikia Watanzania huku ikiahidi ushirikiano katika ujenzi wa taifa Tanzania.
“Tangu umeingia madarakani Machi,mwaka 2021,tumeona mabadiliko chanya ya ukuaji wa sekta ya habari nchini,tunaona uhuru wa kujieleza,upatikanaji wa taarifa na vyombo vya habari unazidi kuongezeka siku hadi siku na tumeshuhudia vyombo vya habari vilivyokuwa kifungoni vimefuguliwa.
Tunatarajia serikali yako itaendelea kusaidia ukuaji wa sekta ya habari,ikiwamo kuendelea kujenga mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara au waliowekeza kwenye vyombo vya habari ili waweze kutoa maslahi mazuri kwa wanahabari”,amesema Kitomari.
“Tunakushukuru wewe na serikali yako kwa kuona changamoto za sheria zinazosimamia taaluma yetu na kuanza kuchukua hatua mbalimbali,ikiwamo mabadiliko ya kanuni ambayo yalikwaza kazi yetu,lakini jitihada zilizopo sasa za kutushirikisha wadau wote wa habari kupitia sheria za habari, ili kuondoa vifungu vinavyokwaza pande zote ni hatua za kutia moyo.Tunaomba wadau wote tushirikishwe kikamilifu”,ameongeza Kitomari.
Amefafanua kuwa licha ya mafanikio mengi kwenye sekta ya habari, bado kuna nitaje changamoto chache zilizopo ambazo zinahitaji ushiriki wa wadau wote na watanzania kuzitatua ikiwemo baadhi ya sheria kuwa kitanzi kwa vyombo vya habari “Tunashukuru hili limeanza kufanyiwa kazi,tunatarajia mabadiliko ya sheria”.
Kitomari amezitaja changamoto zingine kuwa ni hali duni ya maisha kwa waandishi wa habari kutokana na vyombo vingi kushindwa kulipa mishahara kwa wakati au kutolipa kabisa,kwa sababu mbalimbali ikiwamo hali ngumu ya biashara pamoja na Ushindani usio sawa kwenye matangazo kwa vyombo vya masafa ya ndani na vile vya nje,unaochangia kupunguza mapato kwa vyombo vya ndani ambavyo vimeajiri wengi.
Amebainisha kuwa kukosekana utaratibu mzuri utaongeza changamoto ya ajira na kulipa wanahabari,pia ipo changamoto ya kodi ambayo ni kilio cha wamiliki wa vyombo vya habari.
“Changamoto nyingine ni ukuaji wa tekonolojia ulioleta ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni ambavyo vingi maudhui yake haifuati matakwa ya taaluma ya uandishi wa habari na Wananchi kutumia uhuru wao wa kujieleza mitandaoni (Citizen journalism)ambao wakati mwingine unafananishwa na taaluma ya habari kiasi cha wengi kushindwa kutofautisha na kujiita wanataaluma licha ya kutokuwa na vigezo”,ameeleza Kitomari.
“Lakini baadhi wananchi kutumia maudhui hiyo (inayorushwa na wananchi) kuhukumu waandishi wa habari wote kuwa hawajui matakwa ya taaluma yao”,ameongeza Kitomari.
CHANZO: MALUNDE BLOG
No comments:
Post a Comment