WAZIRI NDEJEMBI AAGIZA KITUO CHA AFYA SEGESE KUUANZA KAZI MARA MOJA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 6 October 2024

WAZIRI NDEJEMBI AAGIZA KITUO CHA AFYA SEGESE KUUANZA KAZI MARA MOJA


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius 
Ndejembi alipotembelea  kituo cha afya Segese Halmashauri ya Msalala ambapo amesema kituo hicho kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi  wapate huduma za afya ifikapo mwezi wa kumi na moja


NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL MSALALA


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi amemtaka Mganga Mkuu wa msalala (DMO) kuhakikisha kituo cha afya Segese kinaanza kufanya kazi mara moja kwani jengo la (OPD) tayari limekamilika na vitendea kazi vya kuanzia vipo.


Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo leo octoba 6, 2024 alipotembelea kituo cha Segese na kubaini baadhi ya mapungu ambapo amesema watumishi wanatumia mianya kutokukamilika kwa majengo kupiga fedha za mapato ya ndani.


Aidha Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha amesema Wahandisi wakabidhi majengo yanayolingana na thamani ya fedha zinazotolewa kwani wanapokutwa na changamoto katika majengo yao wanadai kuwa mchoro unatoka wizarani.


Akisoma taarifa za ujenzi wa kituo hicho Mganga Mkuu Dr Sisti Mosha amesema Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2022 kupitia mapato ya ndani shilingi 470,000,000 baada ya wananchi wa Kata Segese kukosa huduma za afya ambapo walianza na ujenzi wa majengo manne, jengo la wagonjwa wa nje OPD, Maabara, Upasuaji na jengo la mama na mtoto.


Ujenzi wa jengo la OPD limegharimu kiasi cha shilingi 208,839,549.9 ambapo umekamilika kwa asilimia 96 na asilimia zilizobaki ni kuingiza umeme, maji na thamani.


Kituo hicho kikikamilika kinatarajiwa kuhudumia wakazi 36,247 wa Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala.


Jengo la mama na mtoto lililokamilika kwa asilimia 70 na kugharimu shilingi 77,501,992.32
Jengo la maabara na OPD ambayo yamekamilika kwa asilimia 96 ambapo jengo la maabara limegharimu shilingi 96,957,632.58 na jengo la wagonjwa wa nje OPD Limegharimu shilingi 208,839,549.9
Waziri Ndejembi akizungumzia swala la kituo cha afya kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi waanze kupata huduma za afya ifikapo mwezi wa novemba
Waziri Ndejembi akizungumzia swala la kituo cha afya kuanza kufanya kazi kwani baadhi ya majengo yako tayari hivyo wananchi waanze kupata huduma za afya ifikapo mwezi wa novemba

Mkuu wa mkoa Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha afya Segese ambapo amewataka wahandisi kukabidhi majengo kulingana na hadhi ya fedha zilizotolewa
Mkuu wa mkoa Anamringi Macha akizungumza katika kituo cha afya Segese ambapo amewataka wahandisi kukabidhi majengo kulingana na hadhi ya fedha zilizotolewa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso