NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wagombea wa nafasi za uenyekiti na ujumbe wa serikali za mtaa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Mhongolo, Manispaa ya Kahama, wamekamilisha zoezi la kurejesha fomu zao leo, Oktoba 31, 2024 ili kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Mhongolo, Juliana Bruno, amesisitiza umuhimu wa wananchi katika kuchagua viongozi wao ambapo amesema kuwa ni wajibu wa viongozi kuwasikiliza wananchi na kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa makandokando na chuki.
Wagombea waliorejesha fomu katika kata ya Mhongolo ni pamoja na Emanuel Nangale kwa uenyekiti na Renatus Thomas, Sharifu Said, Rhoda Josephat, Mariam Seleman, na Quismas Maganga kwa ujumbe.
Katika mtaa wa Nyashimbi, Emmanuel Lutonja ni mgombea wa uenyekiti, huku Juma Sama, Shilinde Idd, Bundala Joseph, Shani Mathias, na Asteria Lameck wakigombea ujumbe.
Juliana amehimiza umoja na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.
No comments:
Post a Comment