TANZANIA NA UINGEREZA WADUMISHA UHUSIANO WA MIAKA 60 YA KIDIPLOMASIA KWA KUWAENZI MABALOZI WASTAAFU. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 23 October 2024

TANZANIA NA UINGEREZA WADUMISHA UHUSIANO WA MIAKA 60 YA KIDIPLOMASIA KWA KUWAENZI MABALOZI WASTAAFU.



Wakati mataifa ya Tanzania na Uingereza yakiadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa Kidiplomasia, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza umeratibu zoezi la uwasilishaji wa Memorabilia kwa Waheshimiwa Mabalozi wastaafu waliowahi kuhudumu katika kituo cha London Uingereza. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Protea Oysterbay jijini Dar es Salaam kama sehemu ya kukumbuka na kuenzi michango yao mikubwa katika kukuza uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Uingereza.


Zoezi la ugawaji wa kumbukumbu kwa Waheshimiwa Mabalozi hao limefanyika tarehe 22 Octoba, 2024 na kuongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mabalozi Wastaafu (ARTA), Balozi Aziz Mlima akiambatana na wawakilishi wawili kutoka ARTA na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Naomi Zegezege.


Akizungumza kwa njia ya simu, Mhe. Balozi Kairuki aliwashukuru Mabalozi husika/ Wawakilishi wao kwa kushiriki katika hafla hiyo pamoja na kuahidi kuendelea kuenzi kazi zao nzuri zilizoacha alama ya ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza kwa kuzifanya kuwa endelevu.


Zoezi hilo linafanyika sambamba na maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Uingereza mwaka huu 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso