MCHENGERWA AWAONYA VIONGOZI WANAOWAONDOA WANANCHI KWENYE MAENEO YA MALISHO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 5 October 2024

MCHENGERWA AWAONYA VIONGOZI WANAOWAONDOA WANANCHI KWENYE MAENEO YA MALISHO




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaonya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaowashawishi na kutaka kuwaondoa wananchi wanaoishi maeneo ya malisho ambayo Serikali ilisharidhia na kutoa tangazo la Serikali ( GN) kuruhusu wananchi hao waendelee kuishi maeneo hayo.




Aidha amesema amesikia kwenye baadhi ya maeneo mkoa wa Arusha kuna mchakato wa kuwaondoa wananchi kwenye maeneo hayo huku wengine wakiwashawishi na kutumia sauti ya Rais kwamba anawataka waondoke kwenye maeneo hayo wakati siyo kweli.




Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo jana katika ziara yake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuzitaja wilaya za Arumeru,Monduli,Karatu,Longido na Ngorongoro kuwa kuna baadhi yao wamekuwa wakiwashawishi na kutaka kuwaondoa wananchi katika maeneo hayo wakidai yanapimwa kwa ajili ya matumizi mengine.




Kutokana na hilo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kusimamia wilaya hizo na kuwa Serikali ilishatangaza GN na maeneo hayo mchakato wa uchaguzi unaendelea ikiwemo kujiandikisha.




Alisema Serikali haitasita kumchukulia hatua kiongozi yoyote atakayehusika na mchakato wa kuwaondoka wananchi wanaoishi katika maeneo ya malisho.




"Wakuu wa wilaya za Arumeru,Monduli, Karatu, Longido na Ngorongoro tuna changamoto ya suala la malisho,wapo wananchi ambao mmewataka wahame kwenye maeneo yao,maelekezo yangu ndiyo maelekezo ya Rais na GN inapotolewa hiyo ndiyo mipaka halali ya wananchi,




"Hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kuwaondoa wananchi mpaka pale mipaka hiyo itakaporekebishwa na Waziri wa Tamisemi,maeneo hayo tumeridhia wananchi wapige kura,bahati nzuri GN tumesoma hapa Arusha,"




"Nasikia kuna michakato wa kuwaondoa wale wananchi kwenye maeneo ya malisho mnaendelea na taratibu za kuwaondoa,kuwashahishi wengine mnatumia mpaka sauti ya Rais kwamba ametaka waondoke huko ni kumchongisha Rais na wananchi,nawaelekeza wakuu wa wilaya nisisikie kiongozi yoyote wa Serikali za Mitaa anawaondoa wananchi ,"ameongeza

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso