NAWAPONGEZA SANA TANROADS KWA KUANZISHA MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE BANGO ZA MIRADI YA MAENDELEO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 23 September 2024

NAWAPONGEZA SANA TANROADS KWA KUANZISHA MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE BANGO ZA MIRADI YA MAENDELEO










Na. Paul Kasembo, SHY RS.


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezindua Bango jipya linaloelezea utekelezaji wa mradi wa barabara ya Kahama hadi Kakola ambalo limeandikwa kwa lugha ya kiswahili ikiwa ni utekelezaji wa ushauri wake wa kuanza kutumia lugha ya kiswahili katika bango zote za miradi ndani ya Mkoa wa Shinyanga kwakuwa miradi yote ni ya wananchi ambao kimsingi wanapaswa kuelewa nini kimeandikwa na nini kinatekelezwa na Serikali katika maeneo yao.




RC Macha ameyasema haya leo tarehe 23 Septemba, alipokuwa akifungua bango hili ambalo limetayarishwa na kuwekwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga kwenye mradi wa ujenzi wa Kilometa 73 Kakola, Bulyanhulu hadi Kahama kwa kiwango cha Lami itakayogharimu zaidi ya Bilioni 101 na itakayotumia miezi 27 kukamilika kwake.




"Nawapongeza sana TANROADS Mkoa wa Shinyanga chini ya Mha. Joel Mwambungu kwa kuwa wa kwanza kutekeleza ushauri wangu wa kuanza kutumia lugha ya kiswahili katika bango zote zinazoelezea miradi inayotekelezwa kwa wananchi ndani ya Mkoa wa Shinyanga, hongera sana Meneja Mha. Joel," amesema RC Macha.




Kuanza kutumika kwa lugha ya kiswahili katika bango zinazoelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ushauri wa RC Macha wa kukienzi, kukitunza na kudumisha matumizi ya lugha ya kiswahili katika maeneo yote hasa kwa bango za miradi ya maendeleo kwa wananchi wetu ambao ni wengi zaidi na ambao ndiyo wenye miradi hii na ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso