SERIKALI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA MITATU YA UONGOZI WA AWAMU YA SITA IMETOA BURE MADUME BORA 361 YA NG’OMBE KWA WAFUGAJI KATIKA HALMASHAURI NANE NCHINI – MATHAYO DANIEL KATIBU MKUU CHAMA CHA WAFUGAJI TANZANIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 25 July 2024

SERIKALI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA MITATU YA UONGOZI WA AWAMU YA SITA IMETOA BURE MADUME BORA 361 YA NG’OMBE KWA WAFUGAJI KATIKA HALMASHAURI NANE NCHINI – MATHAYO DANIEL KATIBU MKUU CHAMA CHA WAFUGAJI TANZANIA




Serikali imetoa bure madume bora ya ng’ombe takriban 361 kwa wafugaji katika halmashauri nane nchini ili kuwawezesha wafugaji kufuga kwa tija.

Akizungumza na wanahabari julai 24, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa awamu ya sita, kwenye sekta ya mifugo, katibu mkuu wa chama cha wafugaji Tanzania Mathayo Daniel amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya sekta hiyo.

“Ndugu wanahabari chama cha wafugaji Tanzania, kinapenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa makubwa aliyoyafanya kwenye sekta ya mifugo, katika awamu hii ya sita tumepokea madume bora ya ng’ombe 361 na kusambazwa kwenye Halmashauri nane hapa nchini, wafugaji wamepewa yale madume kwa vikundi na ni kweli yamekwenda kubadilisha mifugo yao” Alisema Daniel

Ameeleza kuwa serikali pia imenunua ng’ombe 500 zitakazouzwa kwa wafugaji kwa bei nafuu kwa ajili ya kubadilisha kutoka ufugaji usiokuwa na tija na kuanza kufuga ufugaji wenye tija kwao.

“Kama hiyo haitoshi ndugu waandishi wa Habari, serikali ya awamu ya sita imenunua ng’ombe 500 zipo pale Mabuki, zile ng’ombe zinakwenda kuuzwa kwa wafugaji kwa gharama nafuu kwa ajili ya kubadilisha, wafugaji tumekuwa na tabia ya kufuga makundi makubwa, lakini maziwa madogo, ng’ombe hazina tija lakini ng’ombe zilizopo pale unaweza kukuta ng’ombe mmoja anakamuliwa lita kumi hadi kumi na tano, kitu ambacho kwa hawa ng’ombe wetu wa asili unaweza kukuta ng’ombe mmoja anakamuliwa nusu lita, kwa hiyo tumeona ni vizuri sana” Alisema Daniel

Ameeleza kuwa wizara ya mifugo hivi karibuni imeagiza madume bora 60 kutoka Afrika Kusini, ili kuyakopesha kwa wafugaji ambapo kila mfugaji atatakiwa kulipa deni lake ndani ya kipindi cha miaka mitatu, ambayo yatakwenda kuboresha safu za mifugo.

“Juzi tumepokea taarifa na tumeshapeleka wizara ya mifugo, wameagiza madume bora kutoka Afrika kusini, mbegu ambayo kwa mfugaji mmoja kuagiza moja kwa moja kutoka Afrika ya kusuni ni gharama sana, dume moja linaweza kuwa ni milioni 52, lakini serikali ya awamu ya sita imeagiza hayo madume na kuja kukopesha kwa wafugaji, mfugaji anakopeshwa dume analipa ndani ya miaka mitatu, kwa hiyo yale madume yanakwenda kuboresha koo, safu za mifugo maana ukishakuwa na ng’ombe wazuri kwa kweli hautosikia migogoro. Aliongeza

Akizungumzia katika eneo la matibabu ya mifugo, ameeleza kuwa May 20 mwaka huu serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya mifugo imetoa lita 52,000 za kuogeshea mifugo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.4, na kusambaza kwenye mikoa na kupeleka kwenye majosho.

“ Lakini ndugu waandishi wa Habari Tarehe 20 mwezi wa tano wizara ya mifugo imetoa lita 52,000 za kuogeshea mifugo na kusambaza kwenye mikoa na kupeleka kwenye majosho, zina thamani ya bilioni 2.4, ni upendo ulioje kwa serikali ya awamu ya sita kwa wafugaji, kwa hiyo mama Samia amefanya kazi kubwa sana katika sekta hii” Alisisitiza Daniel

Daniel amesema kuwa wizara imejipanga pia kwenda kutoa chanjo kwa mifugo, ambayo imeshatangazwa chanjo ya SOTOKA ya mbuzi na ng’ombe itakayozinduliwa mwezi wa nane mwaka huu na kutolewa bure kwa wafugaji.

“Maeneo mengi yametengwa na kumilikishwa kwa wafugaji, mfano ukienda wilayani Mvomero wameanzisha kampeni inaitwa tutunzane, ambapo kupitia kampeni hii, maeneo mengi ya wafugaji yamepimwa na kupewa hati, na yale maeneo mengi ya wafugaji yamepandwa majani” Alieleza

“Wafugaji wengi hawaamini kuwa kuna majani ya kupandwa, lakini wizara ya mifugo imetoa mbegu ambazo zimepandwa katika mashamba binafsi, karibu kila sehemu nchini, mimi naamini Tanzania iko salama sana, migogoro imepungua kwa asilimia 95” Aliongeza Daniel



“Mimi naamini kwa muendelezo huu ndugu waandishi wa Habari, Tanzania ipo salama, ni kweli kuna changamoto, kwa mfano kuna maeneo ambayo awali yalikuwa ni kinara wa migogoro ya wafugaji lakini kwa sasa iko salama, migogoro imepungua kwa 98%, kwa chama cha wafugaji kwa kushirikiana na serikali katika utatuzi wa hizi changamoto” Alisisitiza Daniel

“Lakini kikubwa ni zile 4R za Mhe Rais, kustahimiliana, kwa kweli tumeona Utanzania umerudi, anapokosea mfugaji, hawajakosea wafugaji wote, amekosea mtu, kwa hiyo kinachofanyika ni kwenda kumdhibiti yule mtu mmoja anayetaka kuchafua taswira, lakini akishadhibitiwa watu wanakaa kichini wanayajenga, yanakwisha, kwa hiyo kwa sasa ile migogoro mikubwa haipo” Alisema

Ameeleza kuwa katika suala la utatuzi wa migogoro limeleta faida kubwa miongoni mwa wafugaji ikiwa ni pamoja na lasi ya maendeleo katika maeneo yote yaliyokuwa na migogoro na kusababisha upendo miongoni mwao.

“Naomba nitoe wito kwa wafugaji wote nchini, waendelee kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, haya mambo anayoyafanya, anayafanya mambo haya kwa nia ya dhati kabisa, kwa hiyo na sisi kama chama cha wafugaji, tunatoa wito, hatupendi kuona umwagaji damu unatokea nchi hii, kwa hiyo tunaomba ikitokea la kutokea, tuache sheria ifate mkondo wake, hakuna sheria imeshawahi kumuumiza au kuondoa uhai wa mtu, mtu atakamatwa, atakaa chini ya ulinzi, na hatua zingine zitachuliwa.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso