PUNGUZA KILO UZUNGUKE KUTATUA KERO ZA ARDHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 26 July 2024

PUNGUZA KILO UZUNGUKE KUTATUA KERO ZA ARDHI


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deo Ndejembi kuhakikisha anazunguka Nchi nzima kutatua kero za Wananchi hata ikibidi kwa kupunguza kilo zake ili awe mwepesi kama Mtangulizi wake Waziri Silaa na kumpa urahisi wa kufanya kazi kwa ufanisi.


Akiongea Ikulu Dar es salaam leo July 26,2024 baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Mh. Ndejembi Waziri wa Ardhi, aliyeondoka (Jerry Silaa) kama nilivyosema amefanya kazi nzuri, kuna hatua alikuwa akichukua za kwenda kutatua migogoro, sasa natazama size ya Jerry na size yako, Jerry alikuwa mwepesi kwenda huko sasa na wewe kilo inabidi zipungue, uzunguke Tanzania nzima kwenda kuifanya kazi hii pamoja na utakaowakuta kule”


“Umefanya kazi nzuri katika kipindi kifupi katika Wizara niliyokutoa, kazi moja nzuri uliyofanya ni ushauri na kushughulika kikamilifu pamoja na Waziri Mkuu shughuli ya kikokotoo ambayo kwa kiasi imetuweka pazuri, sasa nenda kwenye Wizara ya Ardhi kaanzie pale mwenzio alipoishia, kuna masuala ya mradi wa upimaji wa Vijiji wenyewe una masuala mawili matatu mwenzio atakunong’oneza nenda kasimamie vizuri”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso